Uchimu wa Ujerumani waendelea kukua | Matukio ya Kisiasa | DW | 15.08.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Uchimu wa Ujerumani waendelea kukua

Ripoti mpya ya shirrikisho la biashara jumla na ya nje inazungumzia matumaini ya kuzidi kukua uchumi humu nchini

Soko la hisa mjini Frankfurt

Soko la hisa mjini Frankfurt

Uchumi wa Ujerumani unaendelea kukua,lakini sio kwa nguvu kama ilivyokua hapo awali.Hata hivyo ukuaji huo wa kiuchumi una nguvu za kutosha na biashara ya nje nayo pia inanawiri.Kinachotia moyo zaidi ni ripoti za kiuchumi za shirikisho la biashara jumla na ya nje ya Ujerumani,kwa ufupi BGA.Ripoti hizo zinawakilisha masilahi ya makampuni laki moja na 20 elfu yenye wafanyakazi zaidi ya milioni moja na laki mbili.

Si mbaya,hivyo ndivyo ripoti hiyo inavyotafsiriwa na wahusika wa biashara jumla na ya nje ya Ujerumani.Mzozo wa benki zenye kutoa mikopo ya nyumba nchini Marekani waonyesha haukua na madhara makubwa kama ilivyokua ikihofiwa.Mikopo haijapunguzwa na wala haijatathminiwa upya katika tawi lake,anasema mwenyekiti wa shirikisho la biashara jumla na ya nje ya Ujerumani BGA,bwana Anton Börner.Kwa kuingilia kati haraka benki za kimataifa ambazo siku zilizopita zimemimina mabilioni ya fedha,hali kwa bahatio nzuri imeweza kutulia,anasema bwana Börner:

“Ni hali ya kuaminiana kila upande,jambo linalotufanya tukilala tupate usingizi.Hatutarajii madhara yoyote,kwasababu tunaamini fika kwamba benki zina uwezo wa kukabiliana na tatizo la fedha taslim lililojitokeza.Benki zetu hazina shida,kulikua na hali ya kupungukiwa kidogo na fedha taslim kwa muda mfupi.Nnaamini tutaisawazisha bila ya shida yoyote katika kipindi cha wiki nane hadi 12 zijazo.”

Kwa vyovyote vile kivuli kimetanda katika soko la hisa-na haakionyeshi kua kipengee pekee kinachoweza kuutia ila ukuaji wa kiuchumi uliokua ukinawiri hadi sasa. Shirikisho la biashara jumla nay a nje ya Ujerumani BGA tangu muda mrefu uliopita limekua likiashiria kishindo kinachoweza kusababishwa na ile hali ya kudhoofikas sarafu ya dola na kuzidi nguvu sarafu ya Yuro-jambo linaloyatia kishindo makampuni yanayosafirisha bidhaa nchi za nje.Mwenyekiti wa shirikisho la BGA Anton Börner ana tatizo jengine pia linalomshughulisha nalo ni kuzidi kiu cha mali ghafi na nishati ulimwenguni.Bwana Anton Börner anaendelea kusema:

“Ukichanganya pamoja yote hayo,basi hutakosa,kama wewe ni mwanauchumi,kua na msimamo wa wastani kuelekea halai ya siku za mbele.Mie binafsi nnaunga mkono kikamilifu makadirio yaliyotolewa.”

Kwa mujibu wa shirikisho la biashara jumla nay a nje ya Ujerumani BGA,pato jumla la ndani kwa mwaka huu tulio nao litakua kwa asili mia 2.4 tuu.Kiwango hicho ni cha chini ikilinganishwa na mwaka uliopita wa 2006.

Bwana Anton Börner anasema:

“Licha ya hayo hatuna sababu ya kujiwekea matumaini mabaya ya kiuchumi.Kimsingi tunataraji kwamba pato halisi litafikia asili mia mbili nukta tano na mauzo jumla yataongezeka kwa asili mia 4.5 na kufikia jumla ya yuro bilioni 778.Kwa namna hiyo nafasi elfu kumi zaidi za kazi zitapatikana.”

Yanayojivunia zaidi na neema hiyo ni makampuni yanayopsafirisha bidshaa nchi za nje katika wakati ambapo makampuni ya vyakula,vinjwaji,tumbaku na makampuni mengine ya kiuchumi ambayo wateja wake ni wanunuzi wa ndani,yanadorora.

Asili mia 90 ya makampuni yote yanayowakilishwa katika shirikisho la BGA yanaamini chanzo cha hali hii ni cha kisiasa.Wanakosoa zaidi mageuzi ya kodi ya mapato kwa makampuni ,kodi ya marithi na mjadala uliozuka kuhusu kiwango cha mishahara ya chini kinachoruhusiwa kisheria.

 • Tarehe 15.08.2007
 • Mwandishi Kinkartz Sabine/Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CH9W
 • Tarehe 15.08.2007
 • Mwandishi Kinkartz Sabine/Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CH9W

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com