Uchaguzi wa wabunge Iraq | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 07.03.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Uchaguzi wa wabunge Iraq

Uchaguzi wa Iraq umeanza rasmi hii leo . Shughuli ya uchaguzi wa wabunge nchini Iraq imegubikwa na milipuko kadhaa na mashambulio ya makombora baada ya kundi la Al-Qaeda tawi la Iraq kutishia kuivuruga pamoja na kuwaua

Waziri Mkuu wa Iraq Nuri al Maliki anayewania wadhifa huo tena

Waziri Mkuu wa Iraq Nuri al Maliki anayewania wadhifa huo tena

Kiasi cha watu 26 wameuawa mjini Baghad, hii leo baada ya mabomu kulipuka katika maeneo kadhaa.Mashambulio hayo yanavyovilenga vituo vya kupigia kura yameripotiwa pia kutokea katika miji miengine.Zaidi ya wagombea alfu 6 wanawania viti 325 katika Baraza la Wawakilishi wakiwemo wanawake 1.718.Waziri

Selbstmordanschlag in Baghdad, Irak

Hali mbaya baada ya mlipuko wa bomu Baghdad

Mkuu aliye madarakani ambaye ni kiongozi wa chama cha madhehebu ya Shia cha State of the Law Alliance, anawania tena wadhifa huo.Kiasi cha askari polisi na wanajeshi wanapiga doria ili kuwahakikishia wapiga kura usalama.Hii ni mara ya pili, Iraq inafanya uchaguzi tangu utawala wa Saddam Hussein, kuangushwa mwaka 2003 na una azma ya kuutathmini ustawi wake.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com