Uchaguzi wa Berlin | Magazetini | DW | 19.09.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Uchaguzi wa Berlin

Matokeo ya uchaguzi wa Berlin ndio yaliyohanikiza magazetini hii leo.Tuanze na "Markische Allgemeine la mjini Postdam linaloandika:

default

Meya wa Berlin Klaus Wowereit akishangiriwa alipowasili katika ukumbi wa sherehe za chama chake cha SPD mjini Berlin

Serikali ya jiji la Berlin haina kazi ndogo.Inakabiliana na idadi kubwa kupita zote ya wasiookuwa na ajira,watu wengi zaidi wanaopokea msaada wa wakosa ajira wa muda mrefu-Hartz nambari nne,madeni makubwa,hali duni shuleni,juhudi haba za kujumuishwa wageni katika maisha ya kila siku ya jamii,kiu cha matumizi ya nguvu,na mengi mengine yasiyopendeza.Hata hivyo lakini meya ambae yote hayo alilazimika kuyashughulikia,amekuja kuchaguliwa kuendelea na wadhifa wake kwa mara ya tatu mfululizo.Ingawa si ushindi mkubwa hivyo kama ilivyotarajiwa- pigo lakini halikuwa kubwa hivyo.Na hata kama wapiga kura wengi vijana,ambao hawaoni matumaini yoyote kutoka vyama vya jadi vya kisiasa wameamua kukipigia kura chama kipya cha Die Piraten,mradi watu hawawezi kuzungumzia juu ya kuadhibiwa SPD kwasababu ya utawala mbaya.

Wahl Berlin

Mgombea mkuu wa chama cha CDU, Frank Henkel baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa

Gazeti la "Der Tagesspiegel la mjini Berlin lina maoni tofauti na hayo,na linaandika:

Wasoshial Democrats hawana cha kujivunia.mmoja kati ya sita ya wapiga kura wa Berlin ndie aliyekipigia kura chama hicho.Ni idadi ndogo hiyo kwa Klaus Wowereit,inayotokana na idadi ndogo pia ya waliokwenda kutoa sauti zao na matokeo ya wastani ya uchaguzi.Matokeo yake yatakiuka mipaka ya Berlin:Wowereit ,ingawa ataendelea kuwa meya lakini hawezi kutegemea kuchaguliwa kugombea kiti cha kansela kwa tikiti ya chama cha SPD.Hadhi ya mshindi huyo mara tatu wa uchaguzi katika jimbo la Berlin imechujuka kutokana na matokeo ya jana ya uchaguzi,kuweza kupanda katika jukwaa la shirikisho."

Wahl Berlin

Wafuasi wa chama kipya cha Die Piraten

Gazeti la "Cellesche Zeitung linahisi matokeo ya uchaguzi wa Berlin yanaweza kutathminiwa kama hivi:

Kuna washindi chungu nzima.lakini walioshindwa ni wawili.Wakitengwa Die Linke na FDP,wote wengine wanaweza kujinata wameibuka na ushindi.SPD wataendelea kutawala licha ya kupoteza kura,CDU na walinzi wa mazingira Die Grüne wamejikusanyia kura zaidi na chama kipya cha Die Piraten kinaingia kwa kishindo katika bunge la jimbo la Berlin.Waliondolewa patupu si peke yao wafuasi wa siasa kali za mrengo wa shoto-Die Linke,bali pia waliberali wa FDP.Die Linke imepoteza kwa namna hiyo nafasi yake katika serikali ya muungano ya jimbo la Berlin huku FDP ikijikuta nje ya bunge la jiji hilo.