Tunakuunga mkono Rais wa Liberia! asema Clinton | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 14.08.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Tunakuunga mkono Rais wa Liberia! asema Clinton

Marekani imetangaza kuwa inamuunga mkono Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf anayekabiliwa na shinikizo za kujiuzulu.Hayo ni kwa mujibu wa Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton.

default

Waziri wa mambo ya nje wa marekani Hillary Clinton akikamilisha ziara ya Afrika

Marekani imetangaza kuwa inamuunga mkono Rais wa Liberia Ellen Johnson-Sirleaf aliye kiongozi wa kike pekee wa ngazi hiyo barani Afrika.Kauli hizo zimetolewa na Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton aliye katika kituo chake cha sita cha ziara ya bara la Afrika.

Kulingana na Bibi Clinton Marekani imefurahishwa na hatua zilizopigwa na Liberia chini ya uongozi wa Rais Ellen –Johnson Sirleaf.Bibi Clinton alisisitiza kuwa Liberia iko katika mkondo wa sawa na Marekani itaendelea kuiunga mkono nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Ellen Johnson-Sirleaf Präsidentin Liberia

Rais wa Liberia Ellen Johnson-Sirleaf

Rais Sirleaf anashinikizwa kujiuzulu baada ya Tume ya kitaifa ya Ukweli na Maridhiano kupendekeza apigwe marufuku kushiriki katika siasa nchini humo kufuatia madai ya kushirikiana na wababe wa kivita wakati Liberia ilipokabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.Bibi Sirleaf kwa upande wake ameyakanusha madai hayo.Hillary Clinton anatarajiwa kuihitimisha ziara yake ya siku 11 barani Afrika kisiwani Cape Verde hii leo.

 • Tarehe 14.08.2009
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/J9Ok
 • Tarehe 14.08.2009
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/J9Ok
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com