1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump asifu msimamo wa Ujerumani katika vita vya Iran

4 Machi 2026

Rais wa Marekani Donald Trump mjini Washington. Katika mazungumzo hayo yaliyogubikwa na mzozo wa vita Mashariki ya Kati, Trump ameisifu Ujerumani kwa kwa msimamo wake kuhusu vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

https://p.dw.com/p/59m0a
Washington D.C. Marekani 2026 | Rais wa Marekani Donald Trump na Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz na Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Andrew Caballero-Reynolds/AFP

Wakati wa majadiliano kati ya wawili hao, Rais Trump ameipongeza Ujerumani kwa msimamo wake kuhusu vita vya Iran akisema Marekani haihitaji vikosi vya mshirika wake huyo kuwapeleke wanajeshi kuisaidia bali amesisitiza washirika wa NATO kuendelea na mgawanyo wa majukumu ndani ya Jumuiya hiyo unaojikita kwenye aina tofauti za kusaidiana.

Katika mkutano huo uliofanyika Jumanne, Trump amezikosoa Uingereza na Uhispania ambao ni mwanachama wa NATO kwa kuizuia Marekani kutumia kambi zake za kijeshi katika vita dhidi ya Iran. Amesema tabia iliyooneshwa na Uingereza ni ya kushangaza na ametishia kusitisha ushirikiano wake wa kiuchumi Uhispania.

Kwa upande wake Kansela wa Ujerumani ameipinga hatua hiyo lakini nchi yake imeiruhusu Marekani kuendelea kutumia kambi ya kijeshi ya Ramstein. Hata hivyo amekataa kuhusika moja kwa moja kijeshi katika mzozo huo.

Licha ya Merz kuonesha kukubaliana na haja ya kuuondoa utawala wa Iran madarakani, ameweka bayana wasiwasi wake kuhusu mkakati wa Marekani wa kuiongoza Iran baada ya vita.

Merz ataka shinikizo zaidi dhidi ya Urusi

Mara baada ya mazungumzo hayo Merz alizungumza na wanahabari ambapo alitoa wito kwa Trump kujikita zaidi katika kuvimaliza vita vya Ukraine na kumsisitiza aongeze zaidi shinikizo dhidi ya Urusi.

Kansela Merz akiwa Ikulu ya Marekani mjini  2026 | Bundeskanzler Merz im Oval Office
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz 03.03.2026 Picha: Win McNamee/Getty Images

Alisema kuwa, "Urusi inachelewesha mambo kwa kuvuta muda hivyo inakwenda pia kinyume na matakwa ya Rais wa Marekani. Wakati wa mazungumzo, nilisisitiza kuiwekea zaidi shinikizo Moscow. Baada ya miaka minne ya vita, ni wazi uchumi wa Urusi unaonekana kudhoofika. Jeshi la Urusi limepata idadi kubwa ya vifo ambayo haikutarajiwa. Urusi imedhoofika na ndiyo maana tunataka kupata suluhisho lambalo linaishirikisha Ulaya. Hatuko tayari kukubali makubaliano ambayo hatujahusishwa."

Awali, wakati wa mazungumzo ya wawili hao Trump alitilia mkazo kuwa moja ya vipaumbele vyake vikubwa ni kuumaliza mzozo hup huo huku akielezea chuki kubwa kati ya Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

Aidha, Kansela Merz ametumia fursa ya mazungumzo hayo kuzungumzia mivutano ya kiuchumi kati ya Marekani na Umoja wa Ulaya. Alimpatia Trump nakala ya mkataba wa mwaka 1785 wa biashara na urafiki kati ya Marekani na Prussia iliyokuwa sehemu ya Ujerumani. Makubaliano hayo yalikuwa mkataba wa kwanza wa biashara wa kimataifa  kati ya pande hizo mbili.