TOKYO : Merkel akutana na Mfalme wa Japani | Habari za Ulimwengu | DW | 30.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TOKYO : Merkel akutana na Mfalme wa Japani

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amekutana na Mfalme Akihito wa Japani katika kasri la mfalme mjini Tokyo na kuzungumzia mabadiliko ya hali ya hewa,utunzaji wa mazingira na uendelezaji wa matumizi ya nishati mbadala.

Mfalme wa Japani ambaye mara ya mwisho aliitembelea Ujerumani hapo mwaka 1993 ameelezea utashi wa kuendelea kuwepo kwa uhusiano mzuri kati ya Japani na Ujerumani.Mkutano na Mfalme Akihito umepewa kipau mbele wakati wa ziara ya kwanza ya Merkel nchini Japani.

Hapo jana Merkel alikutana na Waziri Mkuu wa Japani Shinzo Abe na kuahidi kwamba nchi zao zitakuwa mstari wa mbele katika juhudi za kupunguza utowaji wa gesi zenye kuathiri mazingira ambao kwa kiasi kikubwa hulaumiwa kwa kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ujoto duniani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com