TEHRAN : Wanafumzi waunguza picha za Ahmedinejad | Habari za Ulimwengu | DW | 11.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TEHRAN : Wanafumzi waunguza picha za Ahmedinejad

Madarzeni ya wanafunzi wa Iran wamezichoma moto picha za Rais Mahmoud Ahmedinejad na kurusha fataki katika juhudi za kuvuruga hotuba yake katika chuo kikuu leo hii.

Hii ni mara ya kwanza kwa rais huyo aliechaguliwa kwa ushindi mkubwa hapo mwezi wa Juni mwaka 2005 kukabiliana na uhasama wa wazi katika tukio la hadhara.

Msemaji wa ofisi ya rais amesema Ahmedinejad hakutibuliwa na tukio hilo na kwamba alimalizia hotuba yake kwenye chuo kikuu cha Amir Kabir mjini Tehran.

Takriban wanafunzi 60 walishiriki katika tukio hilo na hata kudiriki kupiwa mayowe ya Kifo kwa Dikteta.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com