TEHRAN : Iran kuharakisha shughuli za nuklea | Habari za Ulimwengu | DW | 25.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TEHRAN : Iran kuharakisha shughuli za nuklea

Serikali ya Iran imesema itaharakisha ufungaji wa mashinepewa 3,000 kwa ajili ya kurutubisha uranium kufuatia uamuzi wa Umoja wa Mataifa kuiwekea vikwazo nchi hiyo kutokana na mpango wake wa nuklea.

Gazeti la msimamo mkali la Kayhan la Iran limemkariri mjumbe wa Iran katika mazungumzo ya nuklea Ali Larijani akisema kwamba shughuli kwenye mtambo wa urutubishaji wa Natanz nchini Iran zitaendelea kwa mwendo wa kasi kabisa.

Rais Mahmoud Ahmedinejad amesema wale waliounga mkono azimio hilo la Umoja wa Mataifa watakijutia kitendo chao hicho cha ubabaishaji.

Azimio la Umoja wa Mataifa limeziamuru nchi zote kuacha kuipeleka Iran vifaa vyote vinavyohusiana na nuklea pamoja na teknolojia yake halikadhalika linazuwiya mali za kampuni kuu 10 za Iran na watu 12.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com