TBLISI :Mzozo wa Georgia na Urussi wazidi kupanuka | Habari za Ulimwengu | DW | 09.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TBLISI :Mzozo wa Georgia na Urussi wazidi kupanuka

Georgia imeitisha kikao cha dharura cha baraza la usalama la Umoja wa mataifa kujadili kuhusu tukio la Urussi kudondosha mabomu kwenye ardhi ya Geogia. Hata hivyo afisa wake wa ngazi ya juu wa jeshi la anga amesema Urussi haijahusika katika tukio lolote la aina hiyo.Goergia imetisha kikao hicho maalum ikiwa ni siku mbili baada ya tani moja ya makombora kudondoshwa kwenye ardhi yake na kuilaumu Urussi kwa kitendo hicho.Urussi kwa upande wake inasema makombora hayo huenda yalidondoshwa na ndege za Goergia kwa lengo la kutaka kuongeza hali ya wasiwasi kwenye eneo hilo.Umoja wa Ulaya ukizungumzia kuhusiana na mvutano huu wa Goergia na Urussi umezitaka pande zote mbili kujiuzuia na vitendo vitakavyoweza kuzusha hali mbaya.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com