TASHMENT: Waziri wa Ujerumani Walter Steinmeier kuitembelea Uzbekistan | Habari za Ulimwengu | DW | 01.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TASHMENT: Waziri wa Ujerumani Walter Steinmeier kuitembelea Uzbekistan

Waziri wa masuala ya nchi za nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier, amewasili nchini Uzbekistan, ikiwa ni hatua ya pili ya ziara yake ndefu katika 5 za eneo la Ashia ya kati. Waziri Steinmeier amepangiwa kuwa na mazungumzo na viongozi wa Uzebekistan kabla ya kuendelea na ziara yake. Suala la haki za binaadamu ndilo litatwama kwenye mazungumzo katika nchi hiyo mojawapo ya Sovieti ya zamani. Mnamo mwezi Mei mwaka uliopita, waandamanaji 700waliuawa na polisi kulingana na makundi ya kutetea haki za binaadamu. Mwito wa kufanyika uchunguzi juu ya mauaji hayo uliotolewa na Umoja wa Ulaya ulitupiliwa mbali na serikali ya Uzbekistan. Ujerumani ina kituo chake cha kijeshi huko Termes nchini Uzbekistan ambacho kinasiadia kwa nyezo wanajeshi wa Ujerumani katika kikosi cha wanajeshi wa jumuiya ya NATO cha kuweka amani nchini Afghanistan ISAF kwa ufupi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com