1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tajani: Marekani yasema iliarifiwa mashambulizi ya Israel

19 Aprili 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia, Antonio Tajani, amesema Marekani iliuambia mkutano wa kundi la G7 kwamba ilipokea dakika za mwisho taarifa kutoka Israel kuhusu hatua yake ya kurusha droni nchini Iran.

https://p.dw.com/p/4ezK0
Iran, Isfahan
Mojawapo ya maeneo yanayohifadhi mpango wa nyuklia wa Iran, mjini Isfahan.Picha: Atta Kenare/AFP/Getty Images

Waziri mkuu huyo wa Italia, ambayo alikuwa anaongoza mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa kundi la G7, alisema Marekani ilitowa taarifa katika kikao cha asubuhi ya Ijumaa (Aprili 19) ambacho kililazimika kubadili ajenda dakika za mwisho kuzungumzia shambulio linaloshukiwa kufanywa na Israel. 

Soma zaidi: Israel yaishambulia Iran

Taarifa zinasema mapema subuhi ya Ijumaa, Iran ilifyetuwa mifumo yake ya ulinzi wa anga kwenye kambi yake kubwa ya kijeshi na karibu na eneo lenye shughuli zake za nyuklia mjini Isfahan, baada ya kugunduwa droni kadhaa.

Katika tamko la mwisho la kuufunga mkutano wa Capri, mawaziri hao wa G7 walionya kwamba walikuwa wanajiandaa kuiwekea vikwazo Iran na kuzitolea mwito pande zote kujiepusha kuutanua mgogoro.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW