SYDNEY: Bush ahimiza demokrasia katika nchi za Asia | Habari za Ulimwengu | DW | 07.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SYDNEY: Bush ahimiza demokrasia katika nchi za Asia

Rais George Bush wa Marekani ametoa mwito juu ya kuimarisha demokrasia katika bara la Asia.

Akizungumza mjini Sydney kabla ya kuanza mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi za Asia na Pacific rais Bush amesema kuwa nchi zote huru zinapaswa kushirikiana katika kuunga mkono taasisi za kidemokrasia.

Ameitolea mwito serikali ya kijeshi ya Burma iwaachie wafungwa wote wa kisiasa ikiwa ni pamoja na kiongozi wa upinzani Aung San Suu Kyi.

Rais Bush pia atakutana na rais Vladmir Puttin wa Urusi wakati mvutano baina ya nchi zao unaongezeka.

Wakati huo huo rais Vladmir Puttin ametia saini mapatano ya kununua madini ya Uranium kutoka Australia kwa ajili ya vinu vya nyuklia vya nchi yake.

Rais Puttin alitiliana saini na waziri mkuu wa Australia John Howard.

Hata hivyo wapinzani wa mapatano hayo wameeleza wasiwasi juu ya uwezekano wa kuyatumia madini hayo kwa shabaha za kijeshi.

Juu ya wasiwasi huo waziri mkuu Howard ameeleza.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com