Sherehe za X-mas kote duniani | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 25.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

IDHAA YA KISWAHILI

Sherehe za X-mas kote duniani

---

BERLIN

Rais Hörst Kohler wa Ujerumani ameitaka jamii ya wajerumani wakubwa kwa wadogo kushikamana na kushirikiana katika masuala mbali mbali.Katika hotuba yake ya kusherekea Xmas rais Kohler amewashukuru wazee kwa wadogo kwa mchango wako kwa taifa na pia amekiri kwamba ulimwengu umekuwa mgumu zaidi na kwamba gharama za maisha na kodi ziko juu.Aidha ametoa shukurani kwa wanajeshi wa Ujerumani wanaofanya kazi wakati kama huu wa sherehe za Xmas,polisi na wafanyikazi wa mashirika ya misaada wanaofanya kazi nchi za nje kwa ajili ya kutafuta amani ulimwenguni.Wakati huo huo viongozi wa makanisa nchini Ujerumani wametoa mwito wa kusaidiwa kwa watu wasio na uwezo katika jamii na hasa watoto.Na huko Vatican makao makuu ya kanisa Katoliki duniani baba mtakatifu Benedikti wa 16 alifanya ibada ya usiku katika kanisa la mtakatifu peter kama ilivyo destruri.Katika hotuba yake ya Xmas kiongozi huyo wa wakatoliki duniani amewatolea mwito waumini kutafuta wasaa wa kumbuka mwenyezi mungu,wasio bahatika katika jamii na wanaoteseka.Maelfu ya waumini walihudhuria ibada hiyo iliyorushwa hewani mojakwamoja kupitia vituo vya televisheni katika mataifa 42.Aidha katika mji mtakatifu wa Bethlehem ambako inasadikiwa ndiko alikozaliwa yesu Kristo viongozi wa kidini huko wametoa mwito kwa ulimwengu kutenda haki,usawa na kudumisha amani.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com