Sherehe za kuadhimisha miaka 60 tangu kuundwa kwa Jamhuri ya watu wa China | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 01.10.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Sherehe za kuadhimisha miaka 60 tangu kuundwa kwa Jamhuri ya watu wa China

Watu 2,000 walikusanyika katika uwanja wa Tianemen, mjini Beijing, kusherehekea miaka 60 tangu, Jamhuri ya watu ya China ilipoasisiwa.

default

Rais wa China Hu Jintao akagua Gwaride la Kijeshi katika maadhimisho ya miaka 60 mjini Beijing.

Wanajeshi, raia wa kawaida na maafisa wakuu wa chama tawala cha Kikomunisti nchini China waliburudishwa na burudani, ikiwemo gwaride la kijeshi la kwanza nchini China katika
60 Jahr Feiern in China

Shamrashamra za sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya China katika uwanja wa Tianamen Square mjini Beijing

miaka kumi. Rais Hu Jintao alihitimisha sherehe hizo na hotuba muhimu, iliyotoa mafanikio ya nchi hiyo  katika sekta ya uchumi, pamoja na kumwagia sifa tele, Mao Zedong, aliyetangaza kuundwa Jamhuri ya watu wa China, Oktoba Mosi, mwaka wa 1949.

Salamu hizi za hamjambo, marafiki na endeleeni na kazi kwa bidii, masahibu, kutoka kwa Rais Hu Jintao, aliyekuwa amebebwa katika gari lililokuwa wazi, ndizo zilifungua pazia la sherehe za kuadhimisha miaka 60 tangu kuundwa kwa Jamhuri ya watu ya China.

Gwaride kubwa kabisa la kijeshi na vifaa vya kijeshi, ikiwemo, ndege za kivita, vifaru vya kisasa na mitambo ya Satelite ilikuwa wazi kwa kila mmoja kujionea katika sherehe hizi- bila shaka China ilikuwa inataka kutuma ujumbe- tuko imara kijeshi na tunaendelea kuchukuwa nafasi ya ushawishi katika jukwaa la kimataifa.

Raia wa kawaida pia hawakuachwa nyuma katika shamra shamra hizi- zaidi ya laki moja watu waliungana na wanajeshi katika maonyesho yaliyokuwa na ujumbe aina tatu- mafanikio, itikadi pamoja na mtazamo wa baadaye wa Jamhuri ya China.

Rais Hu Jintao, baadaye alikamilisha sherehe za leo , kwa hotuba iliyoonyesha jinsi China ilivyopiga hatua kubwa hasa katika sekta ya uchumi. Hu aliwahakikishia raia wa China kwamba, chama tawala cha Kikomunisti kitaendeleza uchumi wa nchi hiyo, katika misingi ya uhusiano wa jamii  zote kulingana na maadili ya Wachina pamoja na kuhubiri, umoja, utangamano na taifa imara.

Rais Hu Jintao pia alimlimbikizia sifa,

Symbolbild China Klimawandel

Picha ya Mao Zedong, mwasisi wa Jamhuri ya Watu wa China

Mao Zedong, aliyetangaza kuundwa kwa Jamhuri ya China miaka 60 iliyopita. Pamoja na Ze Dong, Hu pia aliwakumbuka viongozi wengine wa chama hicho, Deng Xiapoing na Jiang Zemin akisema wamechangia katika ufanisi wa chama cha kikomunisti na China kwa jumla.

Sherehe za leo zilifanyika katika uwanja wa Tianamen Square, eneo lililokuwa uwanja wa mauti, mwaka wa 89, baada ya mamia ya waandamanaji kuuawa katika maandamano ya kutaka demokrasia nchini China.

Hong Kong ambayo ipo chini ya utawala wa China tangu mwaka wa 97, pia iliadhimisha sherehe hizi, huku kiongozi wa Hong Kong akisema China imekuwa injini ya kusukuma gurudumu la uchumi duniani.

Mwandishi: Munira Muhammad/DPAE

Mhariri: Kitojo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com