SERIKALI YA NIGER ITAMTIA NDANI MTOTO WA GADDAFI, SAADI | Matukio ya Kisiasa | DW | 13.09.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

SERIKALI YA NIGER ITAMTIA NDANI MTOTO WA GADDAFI, SAADI

Niger imesema itamkamata mtoto wa Gaddafi

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Marekani, serikali ya Niger inakusudia kumkamata mtoto wa Gaddafi Saadi aliekimbilia nchini humo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani ameeleza kuwa mapatano yamefikiwa juu ya kumhoji mtoto huyo.

Serikali ya Niger imekubali kushirikiana na Baraza la Mpito la Libya, lakini Saadi hatafutwi kulingana na msingi wa azimio la Baraza Usalama la Umoja wa Mataifa. Na taarifa zaidi kutoka Niger zinasema kuwa watu wengine 31 wa Gaddafi wamekimbilia nchini humo katika siku za hivi karibuni. Hapo awali serikali ya Niger ilihakikisha kwamba itautekeleza wajibu wake wa kimataifa.

Wakati huo huo Mkuu wa serikali ya Mpito ya Libya Mustafa Abdel Jalil kwa mara ya kwanza amewahutubia watu zaidi ya10,000 mjini Tripoli. Bwana Jalil ametaka watu wa Libya wafanye bidii ya kuijenga nchi ya kidemokrasia.

Katika hotuba yake bwana Jalil pia aliusisitiza msimamo wa hapo awali kwamba sheria ya kiislamu inapasa kuwa msingi mpya wa utungaji wa sheria nchini Libya.

Na habari kutoka uwanja wa mapambano zinasema kuwa wafuasi wa Gaddafi wamewaua waasi 15 katika mapigano yaliyotokea kwenye mji muhimu wa mafuta. Akizungumza akiwa amejificha Gaddafi ametoa mwito kwa wafuasi wake wa kuendelea na mapigano jambo ambalo linaashiria kwamba vita vya Libya bado havijamalizika wakati Baraza la Mpito limuefafanua mpango wa kuandikwa katiba na kufanyika uchaguzi katika kipindi cha miezi 20 ijayo.

 • Tarehe 13.09.2011
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/12XhW
 • Tarehe 13.09.2011
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/12XhW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com