Serikali ya Georgia yazima jaribio la mapinduzi | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 05.05.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Serikali ya Georgia yazima jaribio la mapinduzi

Rais Mihel Saakashvili aishtumu Urusi kuhusika na njama hizo ya kutaka kumwondoa madarakani.

Rais wa Georgia Mikhail Saakashvili

Rais wa Georgia Mikhail Saakashvili

Serikali ya Georgia imetangaza imelizima jaribio la mapinduzi lilotaka kufanywa na sehemu ya wanajeshi nchini humo. Rais wa Georgia, Miheil Saakashvili, katika taarifa aliyoitoa kupitia televisheni, ameishtumu Urusi kuhusika na njama hizo za kutaka kumwondoa madarakani na kuiyumbisha Georgia.

Kikosi cha vifaru katika kambi moja ya kijeshi nje ya mji mkuu wa Georgia, Tiblisi, ndicho kilichoandaa uasi huo uliolenga pia kumuua rais Michael Saakashvili. Madai ya Urusi kuhusika na njama hizo yalikanushwa vikali na serikali ya Urusi, hali ambayo imeongeza mvutano wa kibalozi ambao umechipuka tangu vita vya mwezi Agosti mwaka uliopita kati ya majirani hao wawili. Vita hivyo vilichukua muda wa siku siku tano.


Waziri wa ulinzi wa Georgia, David Sikharulidze, amesema uasi huo pia ulilenga kutibua mazoezi ya kijeshi ya Nato yanayotarajiwa kuanza kesho, mbali na kuipindua serikali kwa nguvu za kijeshi. Washukiwa wawili wamekamatwa na rais Saakashvili ametangaza kurejea kwa hali ya utulivu. Akizungumza kuhusu hali hivi sasa nchini Georgia, msemaji katika wizara ya ndani, Shota Uitashvili, amesema


"Hali imedhibitiwa.hivi sasa yanafanyika mazungumzo na makamanda wa vikosi vyote viwili..inaonekana waliohusika wamejisalimisha. Kulikuwa na uasi ambao ulihusisha kikosi kimoja, lakini hivi sasa hali inaonekana kutulia.

Televisheni ya taifa nchini Georgia imetangaza kuwa magari ya doria yalionekana yakielekea katika kambi moja ya kijeshi karibu kilomita 25 kutoka mji wa Tbilisi. Maafisa wa ngazi ya juu nchini Georgia wamesema kisa hicho kilimalizika bila ya machafuko yeyote baada ya wahusika wakuu kujisalimisha. Msemaji wa wizara ya ndani nchini Georgia Shota Uitashvili


"Inavyoonekana mpango ulikuwa kuyatibua mazoezi ya kijeshi ya Nato yaliyopangwa kufanyika kesho; hata hivyo, hali imedhibitiwa na nadhani mazoezi hayo hayatakabiliwa na matatizo yoyote.


Msemaji huyo amesema mipango hasa likuwa kufanywe michafuko ya kijeshi katika sehemu mbalimbali nchini humo.

Georgische Truppen an einem Checkpoint nahe der Stadt Matani

Mwanajeshi wa Georgia akishika doria, karibu na kijiji cha Matani, yapata kilomita 200 kutoka mji mkuu wa Georgia, Tbilisi

Georgia imekabiliwa na kunyumba kwa siasa za nchi hiyo katika muda wa wiki kadhaa, huku makundi ya upinzani yakijaribu kumlazimisha rais Saakashvili ajjiuzulu. Wafuasi wa upinzani wamekuwa wakiandaa mikutano ya hadhara katika mji mkuu kwa karibu mwezi mmoja, kumshinikiza Saakashvili aache madaraka.


Waandalizi wa maandamano hayo walitarajiwa hii leo kuanzisha kampeini nyingine mpya dhidi ya rais huyo, kwa kuweka vizuizi katika barabara kuu , lakini msemaji wa upinzani Sopho Jajanashvili ametangaza kufutilia mbali hatua hiyo.

 • Tarehe 05.05.2009
 • Mwandishi Jane Nyingi/ AFPE..Picha AFP
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/HkLE
 • Tarehe 05.05.2009
 • Mwandishi Jane Nyingi/ AFPE..Picha AFP
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/HkLE
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com