1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROSTOCK: Ghasia zachafua maandamano ya wapinzani wa G-8

3 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBv6

Waandalizi wa maandamano ya kupinga mkutano wa kilele wa G-8 wametuhumu vikali ghasia zilizozuka siku ya Jumamosi mjini Rostock.Takriban watu 1,000 walijeruhiwa katika ghasia hizo.Kwa mujibu wa msemaji wa polisi,kiasi ya polisi 433 walijeruhiwa.Wakati huo huo waandalizi wa maandamano hayo pia wamesema hadi waandamanaji 520 walijeruhiwa na kuongezea kuwa ghasia zilizofanywa haziwezi kuhalalishwa.Siku ya Jumamosi,maelfu ya watu waliandamana kwa amani mjini Rostock,wakitoa mwito wa kulinda mazingira na kutaka misaada bora zaidi kwa nchi zilizo masikini kabisa.Ghasia zilizuka kando ya maandamano hayo baada ya kundi huru kuanza kuwashambulia polisi kwa mawe na mabomu ya petroli.