1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Riadh:Ubalozi wa Marekani Sudan

11 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CEEX

Walinda usalama wa Saudi Arabia, kwa
mujibu wa Wanadiplomasia,
wamewakamata watuhumiwa kadhaa baada
ya mashambulio ya kigaidi
yaliyofanywa mjini Riadh. Gazeti la
lugha ya Kiarabu linalochapishwa
mjini London, Uingereza, "Al-Hayat"
limeripoti kuwa Maafisa wa Usalama
wanazo taarifa zinazowezesha
kukamatwa kwa watu zaidi. Gazeti
jingine linalochapishwa mjini
London, "Al Majalla" limeripoti kuwa
mtandao wa kigaidi wa al-Qaida
umechukua dhamana ya shambulio hilo
kwa njia ya barua pepe. Watu 17
wameuawa miongoni mwao akiwemo
Mkanada katika shambulio hilo
lililofanywa kwenye makazi ya watu
juzi Jumapili. Watu wengine zaidi ya
120 wamejeruhiwa. Serikali ya
Marekani, kutokana na kitisho cha
mashambulio ya kigaidi, imetangaza
kuwa ubalozi wake wa Sudan utafungwa
kwa juma moja kuanzia kesho
Jumatano. Wamarekani wanaoishi
nchini humo wameombwa wawe
waangalifu kupita kiasi.