RANGOON: Kiongozi wa upinzani kukutana na watawala wa kijeshi | Habari za Ulimwengu | DW | 09.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

RANGOON: Kiongozi wa upinzani kukutana na watawala wa kijeshi

Kiongozi wa upinzani nchini Burma,Aung San Suu Kyi yupo tayari kujadiliana na watawala wa kijeshi nchini humo.Katika taarifa iliyosomwa na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa,Ibrahim Gambari,kiongozi huyo wa upinzani amesema,anachukua hatua hiyo kwa maslahi ya umma. Utawala wa kijeshi unatazamia pia kumruhusu mshindi huyo wa zawadi ya amani ya Nobel, kukutana na viongozi wa chama chake kinachogombea demokrasia.Aung San Suu Kyi tangu miongo kadhaa, yupo katika kizuizi cha nyumbani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com