Rais wa Ujerumani kuanza ziara nchini Uturuki
22 Aprili 2024Matangazo
Steinmeier ambaye anazuru Uturuki kwa mara ya kwanza tangu awe rais, amekuwa na mitazamo tofauti na kiongozi wa Uturuki Tayyip Erdogan.
Rais huyo wa Ujerumani alikosoa msimamo wa serikali ya Erdogan kuhusu Israel na pia aliwahi kuibua wasiwasi wake kuhusu mmomonyoko wa kanuni za kidemokrasia nchini Uturuki.
Kituo cha kwanza cha ziara yake itakuwa mji wa Istanbul, ambapo atakutana na wanaharakati wa mashirika ya kiraia, pamoja na meya wa jiji hilo, kiongozi wa upinzani Ekrem Imamoglu, na kisha kukutana na manusura wa tetemeko kubwa la ardhi la mwaka jana huko Gaziantep karibu na mpaka wa Syria. Siku ya Jumatano, Steinmeier anatarajiwa kukutana na Erdogan mjini Ankara.