Rais wa Pakistan atangaza tarehe ya uchaguzi | Habari za Ulimwengu | DW | 19.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Rais wa Pakistan atangaza tarehe ya uchaguzi

Mahakama Kuu nchini Pakistan imeamua,hatua iliyochukuliwa na bunge mwanzoni mwa mwezi wa Oktoba kumchagua Rais Pervez Musharraf kugombea tena uchaguzi wa rais ni halali.Lakini Jaji hakushughulikia mashtaka yanayopinga Musharraf kushika wadhifa wa rais wakati akiwa mkuu wa majeshi.

Musharraf ametangaza kuwa uchaguzi mkuu utafanywa tarehe 8 Januari lakini hakusema lini ataondosha utawala wa hali ya hatari aliotangaza Novemba 3.

Kwa upande mwingine,Imran Khan mwanasiasa wa alietiwa ndani,hii leo ameanza kugoma kula chakula.Yeye anapinga hatua ya Musharraf kuwafukuza kazi majaji,kufuatia tangazo la hali ya hatari.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com