Rais Nicolas Sarkozy aahidi Ufaransa inamuunga mkono Mahmoud Abbas wa Palastina | Habari za Ulimwengu | DW | 30.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Rais Nicolas Sarkozy aahidi Ufaransa inamuunga mkono Mahmoud Abbas wa Palastina

Paris:

Kiongozi wa utawala wa ndani wa Palastina Mahmoud Abbas amezungumzia haja ya kuitishwa uchaguzi katika ukanda wa Gaza chini ya ulinzi wa vikosi vya kimataifa.”Hiyo ndiyo njia pekee ya kuunusuru Umoja wa wapalastina” amesema rais Mahmoud Abbas baada ya mazungumzo pamoja na rais Nicolas Sarkozy mjini Paris.Nchi yake anasema rais Mahmoud Abbas inahitaji sio tuu usalama,bali pia matumaini mema.Rais Nicolas Sarkozy amemhakikishia rais Abbas uungaji mkono wa nchi yake.Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ufaransa Bernard Kouchner amesisitiza utawala wa ndani wa Palastina ndio “wawakilishi pekee halali wa Umma wa Palastina.”

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com