Rais Kikwete asaini sheria mpya ya gharama za uchaguzi
18 Machi 2010Matangazo
Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete, ametia saini sheria ya gharama za uchaguzi ambapo, kwa mara ya kwanza, waandishi wa habari na watu wengine walialikwa kushuhudia tukio hilo katika Ikulu mjini Dar es Salaam.
Sheria hiyo imekosolewa na bwana Jorum Bashange, naibu katibu mkuu wa chama cha wananchi, CUF, Tanzania pamoja na bwana Tundu Lisu, mkurugenzi anayehusika na maswala ya katiba wa chama cha CHADEMA
Mtayarishaji: Josephat Charo
Mhariri: Miraji Othman