1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin asema Urusi itawajuwa walioishambulia

2 Aprili 2024

Rais Vladimir Putin amesema Urusi itagundua ni nani aliyehusika hasa na shambulio la mwezi uliopita kwenye jengo la tamasha karibu na mji wa Moscow ambalo lilisababisha vifo vya watu 144.

https://p.dw.com/p/4eLxV
Urusi | Putin
Rais Vladimir Putin wa Urusi anasema nchi yake itawatambuwa na kuwawajibisha waliohusika na mashambulizi dhidi ya jengo la maonesho karibu na Moscow.Picha: Kremlin.ru/REUTERS

Katika mkutano na maafisa wa wizara ya mambo ya ndani siku ya Jumanne (Aprili 2), Putin alisema watamjuwa aliyeamuru shambulio hilo, huku akiahidi kuwa mchakato huo utafanyika kwa umakini na weledi mkubwa. 

Soma zaidi: Putin: Huenda pia Ukraine ilihusika na shambulizi

Kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu (IS) lilidai kuhusika na shambulio hilo, lakini Urusi inasema washambuliaji walikuwa na mafungano na Ukraine, jambo lililokanushwa vikali na Ukraine pamoja na Marekani iliyosema kuwa ni madai ya kipuuzi.

Hayo yanajiri wakati mapigano makali yanaendelea kati ya Urusi na Ukraine.