1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Polisi yaondoa wanafunzi walioweka kambi kikuu cha Berlin

24 Mei 2024

Polisi nchini Ujerumani imewaondoa karibu waandamanaji 150 wanaowaunga mkono Wapalestina, kutoka chuo kikuu cha mjini Berlin.

https://p.dw.com/p/4gDYZ
Polisi wakiwaondoa kw anguvu wandamaji wanafunzi kutoka kampasi ya chuo kikuu cha Humboldt.
Polisi wakiwaondoa kw anguvu wandamaji wanafunzi kutoka kampasi ya chuo kikuu cha Humboldt.Picha: PRESSCOV/Sipa USA/picture alliance

Polisi nchini Ujerumani imewaondoa karibu waandamanaji 150 wanaowaunga mkono Wapalestina, kutoka chuo kikuu cha mjini Berlin jana, na kukomesha mmoja ya wimbi la mandamano ya wanafunzi barani Ulaya, wanaopinga vita vya Israel Gaza.

Wanaharakati walivikalia vyumba kadhaa vya Taasisi ya Sayansi ya Jamii ya Chuo Kikuu cha Humboldt mjini Berlin siku ya Jumatano.

Soma pia: Wapalestina Rafah wahisi kukwama katikati mwa mashmabulizi ya Israel

Muungano wa Wanafunzi wa Berlin, ambalo ndiyo kundi lililoanda maandamano hayo umekitolea wito chuo kikuu cha Humboldt katika taarifa kubeba jukumu katika kukomesha mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Palestina na mateso yao ya miongo kadhaa.

Maandamano ya wanafunzi kuhusu vita vya Gaza yalioanzia nchini Marekani yamesambaa katika kampasi za vyuo vikuu katika mataifa mengi ya Ulaya. Nchini Ujerumani, maandamano yamefanyika wiki hii kwenye vyuo vikuu katika miji ikiwemo Munich na Leipzig.