1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi wa Ujerumani wakamata mtandao wa ulaghai

Josephat Charo
20 Machi 2026

Mamlaka katika jimbo la Bavaria kusini mwa Ujrumani wamesema leo Ijumaa kwamba wachunguzi wamefunga mtandao mkubwa wa ulaghai kwenye mtandao unaotangaza nyenzo za unyanyasaji wa kingono kwa watoto.

https://p.dw.com/p/5Anze
Polisi wa Ujerumani wakamata mtandao wa ulaghai wa maudhui ya unyanyasaji wa watoto
Polisi wa Ujerumani wakamata mtandao wa ulaghai wa maudhui ya unyanyasaji wa watotoPicha: August Forkel/Bildagentur online/picture alliance

Mamlaka katika jimbo la Bavaria kusini mwa Ujrumani wamesema leo Ijumaa kwamba wachunguzi wamefunga mtandao mkubwa wa ulaghai kwenye mtandao unaotangaza nyenzo za unyanyasaji wa kingono kwa watoto.

Ofisi ya Polisi ya Jinai ya Jimbo la Bavaria, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Bamberg na Wizara ya Sheria ya Bavaria ilisema katika taarifa ya pamoja kwamba msako wa kimataifa unaendelea kwa ajili ya kiongozi anayedaiwa kuwa raia wa China mwenye umri wa miaka 35 anayeishi katika nchi yake ya asili.

Wachunguzi walisema kurasa 373,000 zimeondolewa mtandaoni na kubaini washukiwa 440 kati ya 600.

Kwa zaidi ya miaka minne, wachunguzi wa Bavaria walikuwa wakilenga jukwaa la mtandao ambalo lilikuwa na picha za ukatili mkali wa kingono dhidi ya watoto. Hizi zilitangazwa hasa kwa lengo kuu la ulaghai, ili kuwashawishi wahusika kununua picha na video zaidi.

Waziri wa Sheria wa Bavaria Georg Eisenreich amesema ingawa hizi hazikuwasilishwa hatimaye, maduka bandia yalitangazwa na nyenzo halisi za unyanyasaji wa kingono kwa watoto.