Poland yafanya uchaguzi wa duru ya pili | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 04.07.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Poland yafanya uchaguzi wa duru ya pili

Wananchi nchini Poalnd wanapinga kura katika uchaguzi wa rais uliosababishwa na kifo cha rais wa nchi hiyo Lech Kaczynski katika ajali ya ndege

default

Wagombea urais nchini Poland Bronislaw Komorowski, kushoto, na Jaroslaw Kaczynski, kulia, ambaye ni pacha wa rais wa zamani Lech Kaczynski.

Warsaw.

Wananchi  nchini  Poland  wanapiga  kura  hii  leo  katika uchaguzi  wa  rais  uliosababishwa  na  kifo  cha  rais  wa nchi  hiyo  Lech Kaczynski  kutokana  na  ajali  ya  ndege. Inaonekana  kuwa  uchaguzi  huo  utakuwa  na  ushindani mkubwa  kati  ya  mdogo  wake   marehemu  rais Kaczynski, Jaroslaw,  ambaye  alikuwa  waziri  mkuu  wa zamani,  pamoja  na    rais  wa  muda  mliberali  Bronislaw Komorowski, kutoka  chama  tawala   cha  Civic  Platform. Kura  ya  mwisho  ya   maoni  inaonyesha  kuwa   uchaguzi huo  utakuwa  na  ushindani  mkubwa. Katika  duru  ya kwanza  ya  uchaguzi  hapo Juni  20 , Komorowski  alipata asilimia  41.5  ya  kura , ikilinganishwa  na  asilimia 36.5 alizopata  Kaczynski.  Uchaguzi  wa  leo  unaonekana kuwa  mtihani  muhimu  kabla  ya  uchaguzi  wa  bunge uliopangwa  kufanyika  mwakani  2011.

 • Tarehe 04.07.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OALH
 • Tarehe 04.07.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OALH
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com