Papa aelekea Vatican baada ya kukamilisha ziara Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 21.04.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Papa aelekea Vatican baada ya kukamilisha ziara Marekani

-

NEW-YORK

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa benedikti wa 16 anaelekea Vatican baada ya kukamilisha ziara yake ya siku sita nchini Marekani kwa kufanya ibada maalum ya maombi katika uwanja wa michezo wa Yankee mjini New-York. Awali kiongozi huyo wa kidini alifanya maombi katika eneo kulikotokea mashambulio ya kigaidi septemba mwaka 2001 yaliyosababisha mauaji ya watu kiasi cha 3000.Aidha alizungumza kwa muda mfupi na jamaa za wahanga wa mauaji ya mwaka 2001.Ziara hiyo ya kwanza ya papa nchini Marekani iligubikwa na kashfa ya kulawitiwa watoto kashfa ambayo inawahusisha mapadri wa kikatoli nchini Marekani.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com