PANAMA CITY.Wananchi waunga mkono mpango wa serikali katika kura ya maoni | Habari za Ulimwengu | DW | 23.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PANAMA CITY.Wananchi waunga mkono mpango wa serikali katika kura ya maoni

Wapiga kura nchini Panama wameunga mkono kwa wingi mpango wa serikali wa kutaka kupanua mfereji wa maji wa Panama katika kura ya maoni iliyomalizika.

Asilimia 79 ya raia wa Panama wameunga mkono mpango huo huku asilimia 21 wakipinga wazo hilo.

Wapinzani wa mpango huo waliandamana mwishoni mwa wiki kudai kuwa mradi huo utazidisha deni kubwa kwa nchi hiyo.

Serikali lakini inatetea mpango wake huo wa kupanuliwa kwa mfereji wa maji kwa ajili ya meli za kisasa zipitie katika njia hiyo wakati huu ambapo uchumi wa duniani unapanuka.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com