Olmert na Abbas kujadili hali ya Ukanda wa Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 27.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Olmert na Abbas kujadili hali ya Ukanda wa Gaza

JERUSALEM:

Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert na Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas wanakutana leo hii kujadili hali ya Ukanda wa Gaza.Abbas anatazamia kushauri kuwa maafisa wa serikali yake inayotawala katika Ukingo wa Magharibi wachukue mamlaka ya ulinzi katika eneo la mpakani kati ya Ukanda wa Gaza na Misri na pamoja na Israel pia.Lakini hatua hiyo inahitaji kuidhinishwa na chama cha Hamas kinachodhibiti Ukanda wa Gaza.Wanamgambo wa Hamas siku chache zilizopita walibomoa ukuta wa mpakani kati ya Misri na Gaza na maelfu ya Wapalestina wamemiminika Misri kununua chakula na mahitaji mengine.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com