NOUAKCHOTT:Maandamano ya kupinga bei za vyakula yaua mmoja | Habari za Ulimwengu | DW | 09.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NOUAKCHOTT:Maandamano ya kupinga bei za vyakula yaua mmoja

Yapata mwandamanaji mmoja ameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika maandamano ya ghasia kupinga ongezeko la bei za bidhaa kuu za matumizi.Ghasia zinaripotiw akutokea katika miji kadhaa kusini mashariki mwa Mauritania.Bei za nafaka na mazao mengine zinaripotiwa kuongezeka kwa kiasi kikubwa jambo linalohatarisha maisha ya wakazi wa eneo la Afrika magharibi.Ongezeko la bei za mafuta limesababisha nauli kupanda.

Katika nchi jirani ya Senegal Rais Abdoulaye Wade ameahidi kupunguza idadi ya mawaziri wake aidha kupunguza mishahara ya wafaynikazi wa serikali vilevile wake mwenyewe ili kuunga mkono raia wanaotatizwa na ongezeko la bei za vyakula.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com