NEWYORK.Hakuna dalili za matendo ya kigaidi kufuatia ajali ya ndege ndogo | Habari za Ulimwengu | DW | 12.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEWYORK.Hakuna dalili za matendo ya kigaidi kufuatia ajali ya ndege ndogo

Idara inayosimaia safari za anga na Idara ya usalama ya FBI nchini Marekani zimesema hakuna dalili za matendo ya kigadi kufuatia ajali ya ndege ndogo iliyoangukia katika jengo moja refu la makaazi katika mji wa New York.

Ndege hiyo ilikuwa mali ya mcheza Baseball wa timu ya New York Yankees Cory Lidle aliyekuwa rubani wakati wa ajali hiyo ilipotokea.

Lidle pamoja na mkufunzi wake walikufa katika ajali hiyo.

Wakati huo huo timu ya New York Yankees imetoa taarifa rasmi ya kukiri kifo cha bwana Cory Lidle na imetoa ujumbe wa rambi rambi kufuatia kifo chake.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com