NEW-YORK:Rais wa Iran azikomesha nchi za Magharibi juu ya mradi wake wa Kinuklia | Habari za Ulimwengu | DW | 26.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW-YORK:Rais wa Iran azikomesha nchi za Magharibi juu ya mradi wake wa Kinuklia

Rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad amerudia tena msimamo wake kwamba nchi yake ina haki ya kuwa na technologia ya kinuklia kwa ajili ya matumizi ya amani.

Akihutubia mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini Newyork nchini Marekani rais huyo aliipinga miito mingine ya kuitaka nchi yake ikomeshe shughuli zake za kurutubisha madini ya Uranium akisema Tehran katu haitozisujudia nchi zinazofanya maamuzi yake kwa njia ya kiburi na jeuri kwa kujiona zenye nguvu.

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy akizungumzia juu ya Iran alisema itakuwa hatari kubwa mno ikiwa Iran itaachiwa itengeneze Bomu la Atomiki.Ujerumani pia imezungumzia wasiwasi wake juu ya suala hilo Kansela Angela Merkel akiitolea mwito jumuiya ya kimataifa isigawike juu ya suala la Iran alisema

‚’Sio ulimwengu unaobeba jukumu la kutoa ushahidi kwamba Iran inatengeneza bomu la Atomiki bali ni Iran inayopasa kuushawishi ulimwengu kwamba haina nia ya kutengeneza bomu hilo.’’

Kutokana na mivutano ya muda mrefu kati ya Iran na jumuiya ya kimataifa juu ya shughuli za kinuklia za nchi hiyo Rais wa Iran jana alitangaza katika kikao hicho kwamba mzozo huo wa kinuklia kati ya taifa lake na jumuiya ya kimataifa umekwisha na kwamba sasa upo kwenye mikono ya shirika la kimataifa la kudhibiti technologia ya Kinuklia IAEA.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com