NEW YORK : Umoja wa Afrika na wa Mataifa watafautiana | Habari za Ulimwengu | DW | 21.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK : Umoja wa Afrika na wa Mataifa watafautiana

Hakuna nchi za kutosha zilizotowa wanajeshi wa kulinda amani huko Dafur na Umoja wa Afrika umekuwa ukikwamisha baadhi ya nchi zilizokubali kutowa wanajeshi wao.

Mawaziri au manaibu wao kutoka nchi 26 walikuwa wamealikwa kuhudhuria kikao cha jana usiku kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Alpha Konare kutathmini mipango ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika ya kuweka kikosi cha pamoja huko Dafur,kuyapa nguvu mazungumzo ya amani na kutanuwa msaada kwa zaidi ya watu milioni mbili waliotimuliwa kutoka makaazi yao.

Jean-Marie Guehenno msaidizi katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema mapema wiki hii kikosi hicho bado kinahitaji helikopta maalum,usafiri na vikosi vya usaidizi.

Imeelezwa kwamba Konare alikaata vikosi kutoka Norway, Uruguay na Thailand.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com