NEW YORK: Rais wa Iran aomba kuhotubia Baraza la Usalama | Habari za Ulimwengu | DW | 16.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK: Rais wa Iran aomba kuhotubia Baraza la Usalama

Rais Mahmoud Ahmedinejad wa Iran amepeleka ombi rasmi katika Umoja wa Mataifa kumruhusu binafsi kuhotubia Baraza la Usalama.Hapo awali,nchi tano zenye uanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani, zilikubaliana na mswada wa azimio unaopendekeza kuiwekea Iran vikwazo zaidi,kwa sababu ya kukataa kusitisha mradi wake wa kurutubisha uranium. Mswada huo unataka kupiga marufuku kuiuzia Iran silaha na vile vile kuyashinikiza zaidi kifedha, makampuni yanayoshirikiana na Iran katika miradi yake ya nyuklia na makombora.Mswada huo umewasilishwa kwa wanachama wote 15 katika Baraza la Usalama na utapigiwa kura juma lijalo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com