1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York: Marekani kuwasilisha azimio dhidi ya Burma

28 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCok

Marekani inasema inapanga kuwasilisha azimio mbele ya baraza la usalama la Umoja wa mataifa kuukosoa utawala wa kijeshi nchini Burma, kwa kile inachokiita” kitisho kwa amani na usalama wa kimataifa”. Balozi wa Marekani katika umoja huo John Bolton, alitaja ju ya kushindwa kwa serikali ya Burma kuzuwia biashara ya madawa ya kulevya na binaadamu. Kadhalika alisema kwamba siasa za ukandamizaji za watawala wa kijeshi nchini Burma zimesababisha watu milioni moja kuikimbia nchi hiyo. Balozi Bolton alisema,kwamba Marekani hata hivyo haitotaka hatua ya vikwazo dhidi ya Burma katika azimio hilo la kwanza.