1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Myanmar

Zamani ikiitwa Burma, Myanmar ni nchi inayokutikana Mashariki mwa Asia yenye makundi zaidi ya 100 ya kikabila. Inapakana na India, Bangladesh, China, Laos na Thailand.

Mnammo mwaka 1989 serikali ya kijeshi ilizibadilisha rasmi tafsiri nyingi za majina mengi ya Kiingereza yaliotumika tangu enzi za ukoloni wa Burma, likiwemo jina la nchi lenyewe: "Burma" ikawa "Myanmar". Ubadilishaji huo wa majina umeendelea kuzua mabishano ambapo makundi mengi ya upinzani wa kisiasa na kikabila pamoja na mataifa yanaendelea kutumia "Burma" kwa sababu hawatambui uahalali wa serikali ya kijeshi au mamlaka ya kubadili jina la nchi. Mara baada ya kuchukuwa madaraka Aprili 2016, Aung San Suu Kyi alifafanua kuwa wageni wana uhuru wa kutumia jina lolote kati ya hayo mawili, "kwa sababu hakuna katika katiba yetu, panaposema kwana unalaazimika kutumia neno makhsusi kwa wakati fulani."

Onesha makala zaidi