NEW YORK: Afrika yashikilia ufunguo wa utanuzi wa Baraza la Usalama
24 Julai 2005Matangazo
Mawaziri wa mambo ya nje kutoka Japani,Ujerumani, India na Brazil hapo kesho watakuwa na shinikizo lao la pili la kidiplomasia katika kipindi cha juma moja kutaka kuungwa mkono kuliko muhimu na Afrika kwa jaribio lao kulitanuwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Wagombea hao wanne wa nafasi za kudumu katika Baraza la Usalama wanakutana mjini London hapo kesho na mawaziri wa Umoja wa Afrika kutoka Nigeria,Ghana,Libya, Misri,Algeria na nchi nyenginezo kufikia muafaka juu ya mipango yao inayopingana ya kutanuwa Baraza la Usalama.
Bila ya kuungwa mkono na Umoja wa Afrika wa nchi wanachama 53 hakuna uwezekano wa kutanuliwa kwa baraza hilo la nchi wanachama 15.