NATO ina imani na juhudi za Marekani kusitisha vita Ukraine
2 Desemba 2025
Matangazo
Rutte ameyasema haya wakati ambapo mjumbe maalum wa rais wa Marekani Steve Witkoff yuko mjini Moscow kukutana na Rais Vladimir Putin.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Rutte amesema NATO inakaribisha juhudi zinazoendelea za kuleta amani zikiongozwa na Marekani.
Rutte ameyatoa matamshi haya huku Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy akisema kuwa wajumbe wa Marekani na Ukraine wameubadili mfumo wa mkataba wa amani uliobuniwa mjini Geneva, wakati wa mazungumzo yao ya hivi karibuni yaliyofanyika Florida, Marekani.
Zelenskiy vile vile amesema kuwa anataka mataifa rafiki wa Ukraine barani Ulaya wajumuishwe zaidi katika mchakato huo.