Nani kuongoza operesheni za kijeshi Libya? | Matukio ya Kisiasa | DW | 23.03.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Nani kuongoza operesheni za kijeshi Libya?

Mataifa ya Magharibi yanayoshiriki katika kikosi cha Umoja wa Mataifa kutekeleza marufuku ya ndege kuruka kwenye anga ya Libya, yanajadiliana jinsi ya kuihusisha Jumuiya ya Kujihami ya NATO katika juhudi za kijeshi.

default

Katibu Mkuu wa NATO, Anders Fogh Rasmussen

Lakini bado haijajulikana wazi jinsi muungano huo utakavyohusishwa na nani atakayeongoza operesheni hizo za kijeshi. Rais Barack Obama wa Marekani ana matumaini ya kukabidhi kikosi cha Marekani katika kusimamia operesheni hizo hivi karibuni.

Jana jioni, Rais Obama alisema ana imani kwamba makubaliano yatapatikana katika siku chache zijazo. Baadhi ya nchi ikiwemo Ufaransa na Uturuki zina wasiwasi kuwa kikosi kinachoongozwa na NATO huenda kikaonekana kina sifa mbaya katika ulimwengu wa nchi za Kiarabu. Hata hivyo, muungano huo umekubali kutekeleza vikwazo vya silaha nchini Libya.

Deutschland Japan Bundestag Schweigeminute zum Gedenken an die Opfer

Viongozi wa ngazi ya juu wa Ujerumani, akiwemo Kansela Angela Merkel

Wakati huo huo, Ujerumani imetangaza kujiondoa katika operesheni za Jumuiya ya Kujihami ya NATO katika eneo la Mediterranean kutokana na jeshi la muungano kushiriki katika mzozo wa Libya. Msemaji wa wizara ya ulinzi amesema manowari mbili na meli nyingine mbili zitarejea katika kikosi cha Ujerumani.

Manowari hizo za Lübeck na Hamburg ni sehemu ya operesheni za juhudi za NATO katika kupambana na ugaidi kwenye eneo hilo. Kiasi wanajeshi 70 wa Ujerumani wanaoshiriki katika operesheni za NATO pia wataondolewa.

 • Tarehe 23.03.2011
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/10fz2
 • Tarehe 23.03.2011
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/10fz2
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com