1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvutano wa Goergia na Urussi wazidi kushika kasi

31 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/EAOb

SUKHUMI

Georgia imepinga kwa sauti kubwa hatua ya Urussi hapo jana na leo ya kuepeleka wanajeshi katika jimbo la Abkhazia kusaidia kuimarisha barabara za reli za eneo hilo.Urussi imepeleka maafisa wake 300 wa ulinzi.Hatua hii ndio ya karibuni ambayo inazidisha mvutano kati ya Georgia na Urussi ambayo inaunga mkono madai ya Abkhazia ya kutaka kujitenga.Waziri wa mambo ya nje wa Georgia Grigol Vashadze leo ameishutumu hatua hiyo ya Urussi akisema nchi hiyo inajiandaa kulinyakua eneo la Abkhazia.Urussi ina wanajeshi 2,500 wa kuweka amani Abkhazia eneo ambalo linadhibitiwa na waasi waliojitenga tangu mapema miaka ya tisini.