Muungano wa mirengo ya kati na kulia utafanikiwa? | Matukio ya Kisiasa | DW | 27.09.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Muungano wa mirengo ya kati na kulia utafanikiwa?

Mara ya mwisho Ujerumani ilikuwa na serikali ambayo ina vyama vya mrengo wa kulia na kati ni kati ya kipindi cha mwaka 1982 hadi 1998 wakati wa utawala wa Kansela Helmut Kohl.

default

Bendera za Vyama vya CDU na FDP

Serikali hii mpya inayoungana na chama cha Kiliberali cha FDP inatarajiwa kuwa itaupunguza mchango wa serikali katika hali jumla ya uchumi wa nchi.

Bibi Merkel pia atapata nafasi ya kutoa msukumo katika harakati za kuibatili sheria inayovilazimu viwanda vya nuklia kufungwa katika kipindi cha muongo mmoja ujao.

Katika masuala ya sera za kigeni muungano huu mpya utakuwa na usemi zaidi katika jitihada za kuiwekea Uturuki vikwazo vya kutaka kujiunga na Umoja wa Ulaya.Bibi Merkel anaunga mkono zaidi ushirikiano ulio na manufaa kwa pande zote mbili ila haujumuishi masuala ya uanachama.

Wahlplakat gegen Bundeswehreinsatz in Afghanistan

Bango la Die Linke linalopinga kuwa na vikosi Afghanistan

Uchaguzi huu umefanyika kukiwa na hofu kufuatia vitisho vya kundi la Al Qaeda vilivyotolewa wiki iliyopita vya kuiadhibu Ujerumani endapo wapiga kura wataiunga mkono serikali mpya itakayoendelea kuyaacha majeshi yake Afghanistan.

Ujerumani ina jumla ya vikosi 4200 wanaohusika na shughuli za ukarabati chini ya mwamvuli wa NATO.Chama cha mrengo wa kushoto pekee Die Linke ndicho kinachopinga majeshi hayo kuendelea kubakia Afghanistan.Msikilize mgombea wa chama cha SPD Frank-Walter Steinmeier alichosema pindi baada ya matokeo kutangazwa.

Mwandishi:Thelma Mwadzaya-RTRE/DPAE

Mhariri:Othman Miraji

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com