Musharraf ameahidi uchaguzi ulio huru na wa haki | Habari za Ulimwengu | DW | 15.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Musharraf ameahidi uchaguzi ulio huru na wa haki

ISLAMABAD:

Rais wa Pakistan Pervez Musharraf ameahidi kuwa na uchaguzi ulio huru na wa haki nchini humo Jumatatu ijayo.Hata hivyo ameonya kuwa machafuko yo yote ya kupinga matokeo ya uchaguzi yatazimwa.Wapiga kura siku ya Jumatatu watachagua Bunge la Taifa na mabunge ya wilayani.Ikiwa vyama vya upinzani vitapata wingi wa theluthi mbili basi vitaweza kumshtaki Musharraf alienyakua madaraka kufuatia mapinduzi ya mwaka 1999.Serikali ya Musharraf inatuhumiwa na wapinzani wake kuwa itajaribu kufanya udanganyifu katika uchaguzi ujao. Uchaguzi huo uliahirishwa kutoka tarehe 8 Januari kufuatia mauaji ya kiongozi wa upinzani aliewahi kuwa waziri mkuu,Benazir Bhutto.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com