1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muhtasari wa maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani na A Mtullya

22 Desemba 2005

Mkuu wa benki ya Deutsche Bank bwana Josef Ackermann anafikishwa tena mahakamani kukabiliwa na madai ya kujinufaisha kwa kutoa fidia kubwa kwa watu wa juu katika kampuni ya uhandisi ya Mannesman. Wahariri karibu wote wa magazeti ya Ujerumani wanatoa maoni yao juu ya hayo

https://p.dw.com/p/CBJM

.

Meneja huyo pamoja na watu wengine sita waliidhinisha uamuzi wa bodi ya kampuni hiyo kubwa ya uhandisi juu ya kutolewa fidia kubwa kupita kiasi .

Bwana Ackermann na wenzake ,walifikishwa mahakamani mwaka jana wakikabiliwa na shtaka la kuidhiniisha malipo ya kiasia cha Euro milioni 60.Lakini hawakupatikana na hatia yoyote.

Lakini mahakama sasa imeamua kwamba watu hao wafikishwe tena mahakamani.

Juu ya uamuzi huo mhariri wa gazeti la Die Welt anasema hatua hiyo ni kichekesho kwa kutambua kwamba uamuzi uiliopitshwa mwaka jana juu ya bwana Ackermann na wenzake kuachiwa haukupingwa.Mhariri wa gazeti hilo anauliza jee madhara yapo wapi ?

Lakini mhariri wa gazeti la Mitteldeutsche Zeitung anasema hukumu iliyotolewa mwaka jana sasa ni batili.Mhariri anasema ingawa matokeo ya kesi ya sasa hayajulikani ,hatua ya kuwafikisha tena mahakamani watu hao ni ishara yenye nguvu kwa jamii.Mhariri anasisitiza kuwa ni lazima mameneja , wakurugenzi, na wajumbe wa bodi watambue kwamba tabia ya kujinufaisha haikubaliki.

Mhariri wa gazeti la Rheinnecker katika maoni yake anatumia kauli yenye uwazi zaidi kwa kueleza kwamba uamuzi uliopitishwa mwaka jana kumwachia huru Ackermann na wenzake ulitibua hali ya hewa ya kijamii nchini Ujerumani.Uamuzi huo gazeti linatilia maanani pia uliutia dosari wajihi wa haki nchini.

Nalo gazeti la Süddeutsche Zeitung linasema hatua iliyochukuliwa sasa na mahakama ni tembe chungu kwa mkuu huyo wa benki bwana Josef Ackermann lakini ,katika kipindi cha muda mrefu kijacho, utaleta manufaa kwa Ujerumani ,kwani wajasiriamali watejenga imani ya kuekeza tena vitega uchumi hapa nchini.

Mhariri wa gazeti la Frankfurter Rundschau anasema , kwake siyo tatizo kwa mameneja kupata mishahara mikubwa, la ghasha!Lakini anapinga jambo moja, kwamba vipato vya wastani vya wafanyakazi havijaongezeka sawa sawa wakati mapato ya wakubwa yanasongamana .