1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UtamaduniUjerumani

Msimu wa Kanivali kuongeza kipato cha taifa Ujerumani

9 Februari 2026

Utafiti wa Taasisi ya Uchumi ya Ujerumani (IW) unaonyesha kwamba msimu wa sherehe za Karnevali nchini humo unatarajiwa kuongeza mapato ya taifa kwa takribani euro bilioni 2 mwaka huu huku.

https://p.dw.com/p/58MrL
BdTD | Italien Venedig 2026 | Maskierte Person beim traditionellen Karneval am Kanal
Sherehe za Kanival zatarajiwa kufikia kilele chake wiki hii huku upato la taifa Ujerumani likitarajiwa kuingezeka kutokana na shughuli hizoPicha: Stefano Rellandini/AFP

Utafiti huo ulioonekana na shirika la habari la Reuters, umeonyesha kuwa sekta mbali mbali ikiwemo, hoteli, vilabu vya pombe hadi wauzaji wa mavazi ya kila aina ya kuendana na sherehe hizo zinatarajiwa kunufaika kwa kiwango kikubwa na sherehe hizo.

Lakini licha ya hayo kuripotiwa mapato yatakayopatikana mwaka huu yanasemekana ni chini kwa takriban euro milioni 100 ikilinganishwa na mwaka 2025, kutokana na msimu wa sherehe  hizo kuwa mfupi kwa siku 15 kwasababu ya sherehe za Pasaka safari hii kusherehekewa mapema mwezi wa Aprili.

Tamasha la Carnival nchini Ujerumani huanzia tarehe 11 Novemba (11.11. ), kila mwaka. Tamasha hilo la kitamaduni, ambalo ni maarufu katika miji ya ukanda wa mto Rhine nchini Ujerumani husherehekewa kwa kuvalia mavazi yasiyo ya kawaida, kunywa pombe za aina mbalimbali, kucheza muziki na kufanya kila aina ya starehe.

Deutschland Köln 2025 | Kanivali
Maelfu ya watu wakisherehekea tamasha la Kanivali mjini Cologne, UjerumaniPicha: Martin Meissner/AP Photo/picture alliance

Ni tamasha ambalo hufanywa siku chache kabla ya Jumatano ya majivu, ambayo ndio siku ya kwanza ya kuanza msimu wa Kwaresma wa kufunga siku 40 kwa Wakristo kuelekea sikukuu ya pasaka.

Kulingana na mwanauchumi wa Taasisi ya IW Marc Scheufen, Carnival inatoa nafasi ya siku ya kadhaa za kujiondoa katika habari mbaya na kukumbatia kile kinachowaunganisha watu wote. Ameongeza kuwa hilo halitoi tu nafasi ya kutuliza nafsi yako lakini pia ni faida kwa uchumi wa nchi.

Sekta za kutoa huduma ya chakula kwa mfano zinatarajiwa kuingiaza takriban euro milioni 900 wakati mauzo ya mavazi ya sherehe hizo pamoja na pipi au peremende  zinazotolewa kwa wingi zikitarajiwa kuingiza kiwango cha euro milioni 400. Wasafiri  nao wanatarajiwa kutumia kiasi cha euro milioni 290 kupitia huduma za mabasi na treni na takriban euro milioni 210 kwa malazi ya usiku.

Usalama waimarishwa

Zaidi ya maafisa wa polisi 10,000 walipelekwa kote katika jimbo la North Rhine-Westphalia, na wengine wa ziada wamepelekwa katika maeneo mbali hasa Cologne na Düsseldorf  kuzuwia kile kilichosemekana kuwa ni vitisho vya mashambulizi kutoka kwa watu walio na itikadi kali.

Ujerumani Karneval 2025
Usalama waimarishwa katika maeneo mbali hasa Cologne na Düsseldorf  kuzuwia kile kilichosemekana kuwa ni vitisho vya mashambulizi kutoka kwa watu walio na itikadi kali.Picha: Michael Nguyen/NurPhoto/picture alliance

Maafisa wengine walikuwepo katika maeneo ya ukaguzi wa barabarani ambako walikuwa wanaangalia pochi na mifuko ya wahudhuriaji kwenye sherehe hizo za Kanivali zinazofurika kupita kiasi.

Maafisa hao wanajaribu kuzuwia watu kuingia na vitu kama visu au kitu chochote kinachoweza kutumikakama silaha ili kuepusha purukushani katika sherehe hizo.

Mji wa Cologne ndio kitovu cha sherehe hizo. Sio maeneo yote ya Ujerumani yanayojitosa katika sherehe hizo za Karnival. Miji ya Cologne, Düsseldorf, na Mainz ndio yanayokuwa na mbwembwe zaidi ikifuatiwa na miji mingine ya Munich, Aachen, Bonn, Nuremberg, Stuttgart, Bremen, na Wiesbaden.