Msiba wa hillsbrough-Stadium miaka 20 iliopita. | Michezo | DW | 14.04.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Msiba wa hillsbrough-Stadium miaka 20 iliopita.

Mashabiki 96 wafariki dunia-730 wajeruhiwa.

Fabio Aurelio(kulia) FC Liverpool

Fabio Aurelio(kulia) FC Liverpool

Msiba wa karibuni katika uwanja wa dimba barani Afrika ni ule uliotokea mwezi uliopita mjini Abidjan,Ivory Coast pale timu ya nyumbani ilipocheza na Malawi katika kinyanganyiro cha kuania tiketi za Kombe lijalo la dunia 2010 nchini Afrika Kusini.Jumla ya mashabiki 22 waliuwawa pale ukuta ulipoporomoka kwa kusheheni mashabiki uwanjani mjini Abidjan.

Msiba mkubwa kabisa wa aina hii lakini, ulitokea miaka 20 iliopita siku kama leo huko Shefield,Scotland pale timu mbili za Uingereza zilipokutana uwanjani: Hillsbrough Stadium, April 15 siku kama leo, 1989.Liverpool iliocheza jana usiku na chelsea katika Champions League-kombe la klabu bingwa barani Ulaya, ilikumbana wakati ule na Nottingham forest kuania nafasi ya finali ya Kombe la FA.

Mpambano kati ya FC Liverpool na Nottingham Forest ulikwishaanza kwa muda wa dakika chache pale msiba huo mkubwa katika historia ya kabumbu ya ulaya kutokea uwanjani.

Nafasi za kusimama katika jukwaa la upande wa magharibi la uwanja wa dimba wa Hillsbrough zilikwishasheheni pomoni.Juu ya hivyo,mashabiki zaidi wa FC Liverpool,iliokuwa jana usiku tena uwanjani na Chelsea, wakisonga mbele kutoka nyuma kuingia uwanjani na kukiuka uwa wa ulinzi.Mashabiki waliojaribu kukikuka uwa huo na kuingia uwsanjani kujiokoa,walizuwiliwa na polisi.

Sawa na msiba uliotokea Uwanja wa Heysel Stadium mjini Brussels, miaka 4 kabla ya ajali hii, vikosi vya usalama vilikawia mno kufungua milango mikuu ya uwanjani na kuwaacha mashabiki waliofadhahika uwanjani kwenye majani.Haukupita muda ukubwa wa msiba uliotokea ukaanza kufahamika.

Mashabiki 730 walijeruhiwa,96 walifariki dunia -kati yao wanaume 89 na wanawake 7 na wengi wao hawakupindukia umri wa miaka 20.Chipukizi kabisa alikuwa mtoto wa miaka 10.

Ni baada ya kupita dakika 40 tangu mchezo kuvunjwa ,ndipo ambulance ya kwanza imewasili uwanjani.Lango la kuingilia uwanja huo lilikuwa bado limekomewa kufulu.Ufungo haujulikani ulipo.Mashabiki wa timu zote mbili wakihudumiana na kusaidiana.

Mara tu baada ya mchezo huo vyombo vya habari viliwastupia jukumu la balaa hili m ashabiki wa FC Liverpool.Kwani, ilikuwa mashabiki-wahuni wa Liverpool waliosababisha ule msiba wa miaka 4 kabla katika

Muandishi:Ramadhan ali

Mhariri: Saumu Ramadhan Yusuf