MOSCOW:Puttin asisitiza kuwa Iran hjaina nia ya kutengeneza silaha za nyuklia
11 Oktoba 2007Matangazo
Rais Vladimir Puttin wa Urusi amesema nchi yake haina ushahidi kwama Iran inataka kutengeneza silaha za nyuklia.
Kiongozi huyo ameyasema hayo baada ya duru ya pili ya mazungmzo na rais Nicholas Sarkozy wa Ufaransa ambae anazuru nchini Urusi.
Kufuatia kauli hiyo ya rais Vladimir Puttin huenda nchi za magharibi zikashindwa kupitisha hoja yao ya kutaka Iran iongezewe vikwazo zaidi katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.