MOSCOW : Urusi yafanya uchaguzi wa majimbo | Habari za Ulimwengu | DW | 11.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOSCOW : Urusi yafanya uchaguzi wa majimbo

Wapiga kura wanapiga kura katika chaguzi za serikali za mitaa nchini Urusi ambazo zinaonekana kwa kiasi kikubwa kuwa ni tathmini kwa uchaguzi wa bunge wa mwaka huu na wa urais wa mwaka 2008.

Watu milioni 30 wanastahili kupiga kura katika majimbo 14.

Uchaguzi huo umetiwa dosari na shutuma kwamba vyama vya upinzani vimekuwa vikitengwa kwa makusudi.Vyama vidogo havishiriki uchaguzi huo kutokana na sheria ya kukitowa chama chochote kile ambacho kinashindwa kupata angalau asilimia saba ya kura.

Hii ina maana kwamba uchaguzi utakuwa kwa kiasi kikubwa kati ya vyama vikuu kile kinchounga mkono Ikulu ya Urusi, Chama cha Muungano wa Urusi na kile kinachoitwa Just Russia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com