MOSCOW: Russia na Belarusia zaafikiana kuhusu usambazaji wa mafuta. | Habari za Ulimwengu | DW | 13.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOSCOW: Russia na Belarusia zaafikiana kuhusu usambazaji wa mafuta.

Rais Mwai Kibaki yumo katika juhudi za kuwania tena kiti cha Urais.

Rais Mwai Kibaki yumo katika juhudi za kuwania tena kiti cha Urais.

Russia na Belarusia zimetia saini mkataba rasmi unaotanzua mzozo wa usambazaji wa mafuta ambao ulisababisha kukatizwa kwa huduma za mafuta kupitia bomba moja kuu kuelekea mataifa ya Ulaya.

Duru za habari zimemnukuu Waziri Mkuu wa Russia, Mikhail Fradkov, akisema tofauti zilizokuwepo zimetatuliwa.

Mkataba huo unajumuisha taratibu kadha za biashara ya mafuta ambayo Russia ilikuwa imedai kuwa Belarusia ilikuwa ikijipatia kwa njia ya udanganyifu.

Mzozo huo siku ya jumatatu iliyopita ulisababisha kufungwa kwa siku tatu bomba la kupitishia mafuta kuelekea mataifa ya Ulaya.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com