MOGADISHU:Afisa mkuu wa WFP atekwa na vikosi vya serikali | Habari za Ulimwengu | DW | 18.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISHU:Afisa mkuu wa WFP atekwa na vikosi vya serikali

Shirika la chakula la umoja wa mataifa WFP limesimamisha shughuli za kugawa chakula katika mji mkuu wa Mogadishu nchini Somalia baada ya vikosi vya serikali kuvamia kambi ya umoja wa mataifa na kumteka nyara afisa mkuu wa shirika la WFP katika eneo hilo bwana Idris Osman.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon amelaani kitendo cha kutekwa nyara afisa mkuu huyo na amesema kuwa hatua hiyo imekiuka mkataba wa umoja wa mataifa wa mwaka 1946 ambapo Somalia ni mwanachama.

Katibu mkuu ametoa mwito wa kuachiliwa kwa haraka bwana Osman ambae anazuiliwa katika katika makao makuu ya shirika la upelelezi la Somalia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com